UPENDO DHIDI YA HOFU NA WAJIBU
Nishikapo Amri za Mungu, za Kanisa na kufuata miongozo ya viongozi wangu, nafanya kwa sababu ya upendo au nafanya kwa kuwa ninaogopa kuwa nisipofanya nitaonekana ni mkaidi, jamii haitanielewa na sitaingia Mbinguni? Ninapotoa zaka, kuwasaidia masikini na kufanya kazi za Mungu, Je, ninafanya kwa kutimiza wajibu au ninafanya kwa sababu ninampenda Mungu na jirani? Aghalabu maisha yetu yametawaliwa na hofu juu ya adhabu za Mungu na za jamii na mara nyingi twafanya mambo mengi tukiwa na lengo la kutimiza wajibu wala si kwa sababu ya upendo. Kuishi kwa kuogopa sheria na kufanya mambo mema kwa kutimiza wajibu bila upendo kunachosha na kunaondoa furaha ya jambo zuri tulifanyalo. Lakini pia sifai mbele za Bwana kama nitajisukuma kufanya mambo mema bila upendo (1 Kor 13:1-3). Yesu alipoulizwa kuhusu Amri iliyokuu kupita zote alieleza kwa ufasaha kuwa ni upendo kwa Mungu na kwa jirani (Matahyo 22:36-38) . Yesu kwa mafundisho yake hapa aneleza kuwa upendo ukitawala nafsi, hausukumwi na...