VISAKRAMENTI KATIKA KANISA KATOLIKI
Visakramenti ni nini? Ni alama takatifu ambazo kwa sababu zinafanana na Sakramenti, zinaashiria kupatikana kwa matunda ya kiroho kupitia maombi ya kanisa. Visakramenti huwasaidia watu kupokea tunda la msingi la Sakramenti na mazingira mbalimbali ya maisha hutakaswa. Katika maana nyengine: Visakramenti ni shara takatifu zilizoanzishwa na Kanisa ambazo lengo lake ni kuwaandaa watu kupokea tunda la Sakramenti na kutakatifuza mazingira mbalimbali ya maisha. Mfano wa Visakramenti: Misalaba, Medani, Rozari, Skapulari, Maji ya baraka, Matawi yaliyobarikiwa, Majivu yaliyobarikiwa n.k Visakramenti hufanyikaje? Visakramenti hufanyika kwa njia ya Baraka. Ukiwa na Msalaba, Rozari Skapurari etc ambayo haijabarikiwa ni kazi bure haiweizi kufanya kazi yoyote. Ni baada ya kubarikiwa na Padre ndipo Visakramenti hupata pumzi ya uhai ndani yake. Hivyo twasema ni katika kubarikiwa Visakramenti hufanya hai navyo huweza kutubariki. NB: Kila Mkristo mbatiwa naye alibarikiwa hivyo huitwa ...