KANISA LINAISHI MAFUNDISHO YAKE – MSAMAHA

Fr. Innocent Bahati Mushi OFMCap

Kanisa liko makini juu ya kile ambacho linafundisha. Linajitahidi kadiri iwezekanavyo kutafsiri mafundisho yake kwa matendo. Linafahamu fika kwamba matendo huongea zaidi kuliko maneno matupu. Kanisa kwa lenyewe limekuwa likiomba msamaha kutokana na madhambi na madhaifu ya wanawe. Huu ni utambuzi kwamba Kanisa ni la kimungu lakini pia ni taasisi ya kibinadamu, watu ambao wamejeruhiwa na dhambi ya asili na wana maelekeo ya dhambi.

Wakati wa hija, huko nchi takatifu tarehe 23 Marchi, 2000, Papa Yohani Paulo II alienda Yad Vashem, sehemu ya kumbukumbu ya maangamizi ya Waisrael (Holocost). Huko Papa alisema: 

“Kama Askofu wa Roma, na Khalifa wa Petro, ninapenda kuwahakikishia Wayahudi wote kwamba Kanisa Katoliki, likisukumwa na nguvu ya ukweli na upendo wa kiinjili, bila kuingiza mambo ya kisiasa ndani yake, linahuzunishwa na kusikitishwa na kitendo cha Wakristo, wa wakati wowote na mahali popote, kuwachukia, kuwatesa na hata kuwaua ndugu Wayahudi (Anti-Semitism).[1]

Baada ya kuyasema maneno hayo, tarehe 26 March, Papa alitembelea “Ukuta wa maombolezo”[2] huko Yerusalem. Hapo alisali na kuacha ujumbe akimwomba Mungu awasamehe waliosababisha wana wa Abrahamu kuteseka: Hii hapa ni tafsiri ya ujumbe wa Papa:

“Mungu wa Baba zetu, ulimchagua Abrahamu na warithi wake kulileta Jina lako kwa mataifa, tunasikitika na kuhuzunika kwa tabia ya wale ambao, katika historia, wamesababisha wanao kuteseka, na tukikuomba msamaha, tunanuia kuishi udugu wa kweli na watu wa Agano.”

Papa Yohani Paulo II alifanya, hivyo kwa niaba ya vizazi vyote, kwa sababu anafahamu kwamba, Kanisa linashiriki katika fumbo la Kristo, aliyeteswa, kufa na kufufuka, ambaye alijitwika dhambi za watu wote kwa nyakati zote.[3] Papa anasisitiza kwamba ikiwa tunasameheana ulimwengu utakuwa ni mahali pa amani, tena jamii inajaa fadhila za kiutu.

[1] L’Oservatore Roman N 13-29, March 2000, p 7

[2] Western or “Wailing” Wall.

Popular posts from this blog

IFAHAMU SAKRAMENTI YA KITUBIO/UPATANISHO

IFAHAMU SALA YA BWANA (BABA YETU)

NYIMBO ZA BIKIRA MARIA