Posts

Showing posts from May, 2017

MKRISTO USIOGOPE KIFO JIANDAE KWA KIFO CHEMA

Makala hii ni sehemu ya Kitabu cha Kalamu kwa Vijana ambacho kipo katika hatua za mwisho kuchapishwa.  Haki zote za mwandishi zimehifadhiwa. Utangulizi Kati ya mambo ambayo binadamu tunayaogopa sana mojawapo ni kifo, mwanadamu anaogopa kifo kwa kuwa kwanza kinamtenga na familia yake, ndugu, jamaa marafiki ambao amezoeana nao, pili anaogopa kifo kwa kuwa hafahamu ni wapi anapoelekea, jambo lingine linalowaogopesha watu juu ya kifo ni kuyaacha mambo ya dunia na raha zake ambazo amekua akizihangaikia kwa muda mrefu sana, kifo huogopwa pia kutokana na hukumu kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu na hukumu yake. Mwanadamu anapofariki huku nyuma huacha majonzi na simanzi kubwa haswa kwa wale waliokua wanamtegemea na wote ambao kwa namna moja au nyengine walikua wanafaidika na uwepo wake hapa duniani. Kifo cha kijana mara nyingi huwa ni pigo zaidi, maana ujana ni wakati wa mtu kuchanua na jamii huwa imejiandaa sana kuvuna kutoka kwa vijana, anapofariki kijana jamii huhuzunika zaidi ...

NYIMBO ZA BIKIRA MARIA

Zifuatazo ni nyimbo mbalimbali za Bikira Maria. Bonyeza nyimbo husika na utaweza kuidownload moja kwa moja AVE MARIA BARAGUMU LA MARIA HERI MARIA HESHIMA TWATOA ISHARA KUBWA JINA LA MARIA LITUKUZWE POTE JINA TUKUFU LA MARIA MAMA WA MWOKOZI TUSIKIE WANAO MARIA MWOMBEZI MIMI NI MTUMISHI WA BWANA MKONO WAKO PAMOJA NA MALAIKA MARIA MSIMAMIZI SALAMU MALKIA WA MBINGU SALAMU MAMA MARIA SALAMU MARIA EE MAMA TUMSIFU MARIA ENYI WANAE ULIZALIWA PASIPOKUA NA DHAMBI UNITETEE KWA MWANAO ZIPENDE NYIMBO ZETU Kwa tatizo lolote wasiliana nasi

Akawanyeshea Mana ili wale

Bonyeza hapa kudownload

Neno kwa Vijana

Vijana tukumbuke mitume na manabii wengi walieneza dini na neno la Mungu angali ni vijana, wakiwa wana nguvu na wenye kustawi, nguvu yao hawakuipeleka katika maasi na machukizo kwa Mungu, bali waliutoa ujana wao machoni pa Mungu wakiitenda kazi yake, na wengine walikufa wakieneza dini tena hawakuona maumivu yoyote kwa sababu walifanya kwa mapenzi ya Muumba wao. Kijana ukiwa bado una nguvu usikubali shetani atumie nguvu yako kumuasi Mungu, Mwili wako usitumike kwa uzinzi wala nguvu yako kwa kuiba kwa kunyang’anya, vipaji vyako visiwe chachu ya maovu kwa kuimba na kucheza isivyompendeza Mungu, kichwa chako na kisitumike kutunga na kuandaa hadithi na michezo yenye uovu. Kumbuka nguvu ya ujana wako yaweza kukupa baraka tele kwa Mungu ukiitumia vizuri bali uitumiapo vibaya itakupeleka katika moto wa milele. Kijana tazama shetani ameweka maoteo mbele yako, usiinue macho yako kutazama wanawake waliovaa vibaya maana utawaka tamaa na binti usiwe kichocheo cha tamaa, kinywa chako kisitoe man...