Posts

UPENDO DHIDI YA HOFU NA WAJIBU

Image
Nishikapo Amri za Mungu, za Kanisa na kufuata miongozo ya viongozi wangu, nafanya kwa sababu ya upendo au nafanya kwa kuwa ninaogopa kuwa nisipofanya nitaonekana ni mkaidi, jamii haitanielewa na sitaingia Mbinguni? Ninapotoa zaka, kuwasaidia masikini na kufanya kazi za Mungu, Je, ninafanya kwa kutimiza wajibu au ninafanya kwa sababu ninampenda Mungu na jirani? Aghalabu maisha yetu yametawaliwa na hofu juu ya adhabu za Mungu na za jamii na mara nyingi twafanya mambo mengi tukiwa na lengo la kutimiza wajibu wala si kwa sababu ya upendo. Kuishi kwa kuogopa sheria na kufanya mambo mema kwa kutimiza wajibu bila upendo kunachosha na kunaondoa furaha ya jambo zuri tulifanyalo. Lakini pia sifai mbele za Bwana kama nitajisukuma kufanya mambo mema bila upendo (1 Kor 13:1-3). Yesu alipoulizwa kuhusu Amri iliyokuu kupita zote alieleza kwa ufasaha kuwa ni upendo kwa Mungu na kwa jirani (Matahyo 22:36-38) . Yesu kwa mafundisho yake hapa aneleza kuwa upendo ukitawala nafsi, hausukumwi na

NYIMBO ZA KWARESIMA

Image
Zifuatazo ni nyimbo mbalimbali za kwaresima, unaweza kusikiliza na kudownload, bonyeza wimbo unaoutaka na moja kwa moja ukurasa mpya utafunguka utakao kuwezesha kusikiliza nyimbo hiyo, na juu kabisa kutakua na alama inayokuonesha kudownload bonyeza alama hii ipo juu kabisa. . Ukipata tatizo jaribu kubadilisha browser unayotumia kudownload. Karibu ASIREGEE MOYOWE BWANA KAMA WEWE UNGEHESABU MAOVU YETU BWANA NI KINGA NA NGAO YANGU EE BWANA USIKIE KABILA LANGU KRISTO ALIJINYENYEKEZA KRITO AMEKUA MTII KWA ISHARA YA MSALABA KWA NINI WASIMAMA MBALI LAUMU IMEUVUNJA MATESO YAKO MSALABANI MTAZAME MWOKOZI MUNGU WANGU MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA NIMEKUKIMBILIA PASIPO MAKOSA TUKOMBOE TUMEKOSA KWELI WAKUPELEKA HUKUMUNI YESU WANGU YESU AKALIA KWA SAUTI KUU

MKRISTO USIOGOPE KIFO JIANDAE KWA KIFO CHEMA

Makala hii ni sehemu ya Kitabu cha Kalamu kwa Vijana ambacho kipo katika hatua za mwisho kuchapishwa.  Haki zote za mwandishi zimehifadhiwa. Utangulizi Kati ya mambo ambayo binadamu tunayaogopa sana mojawapo ni kifo, mwanadamu anaogopa kifo kwa kuwa kwanza kinamtenga na familia yake, ndugu, jamaa marafiki ambao amezoeana nao, pili anaogopa kifo kwa kuwa hafahamu ni wapi anapoelekea, jambo lingine linalowaogopesha watu juu ya kifo ni kuyaacha mambo ya dunia na raha zake ambazo amekua akizihangaikia kwa muda mrefu sana, kifo huogopwa pia kutokana na hukumu kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu na hukumu yake. Mwanadamu anapofariki huku nyuma huacha majonzi na simanzi kubwa haswa kwa wale waliokua wanamtegemea na wote ambao kwa namna moja au nyengine walikua wanafaidika na uwepo wake hapa duniani. Kifo cha kijana mara nyingi huwa ni pigo zaidi, maana ujana ni wakati wa mtu kuchanua na jamii huwa imejiandaa sana kuvuna kutoka kwa vijana, anapofariki kijana jamii huhuzunika zaidi hasw

NYIMBO ZA BIKIRA MARIA

Zifuatazo ni nyimbo mbalimbali za Bikira Maria. Bonyeza nyimbo husika na utaweza kuidownload moja kwa moja AVE MARIA BARAGUMU LA MARIA HERI MARIA HESHIMA TWATOA ISHARA KUBWA JINA LA MARIA LITUKUZWE POTE JINA TUKUFU LA MARIA MAMA WA MWOKOZI TUSIKIE WANAO MARIA MWOMBEZI MIMI NI MTUMISHI WA BWANA MKONO WAKO PAMOJA NA MALAIKA MARIA MSIMAMIZI SALAMU MALKIA WA MBINGU SALAMU MAMA MARIA SALAMU MARIA EE MAMA TUMSIFU MARIA ENYI WANAE ULIZALIWA PASIPOKUA NA DHAMBI UNITETEE KWA MWANAO ZIPENDE NYIMBO ZETU Kwa tatizo lolote wasiliana nasi

Akawanyeshea Mana ili wale

Bonyeza hapa kudownload

Neno kwa Vijana

Vijana tukumbuke mitume na manabii wengi walieneza dini na neno la Mungu angali ni vijana, wakiwa wana nguvu na wenye kustawi, nguvu yao hawakuipeleka katika maasi na machukizo kwa Mungu, bali waliutoa ujana wao machoni pa Mungu wakiitenda kazi yake, na wengine walikufa wakieneza dini tena hawakuona maumivu yoyote kwa sababu walifanya kwa mapenzi ya Muumba wao. Kijana ukiwa bado una nguvu usikubali shetani atumie nguvu yako kumuasi Mungu, Mwili wako usitumike kwa uzinzi wala nguvu yako kwa kuiba kwa kunyang’anya, vipaji vyako visiwe chachu ya maovu kwa kuimba na kucheza isivyompendeza Mungu, kichwa chako na kisitumike kutunga na kuandaa hadithi na michezo yenye uovu. Kumbuka nguvu ya ujana wako yaweza kukupa baraka tele kwa Mungu ukiitumia vizuri bali uitumiapo vibaya itakupeleka katika moto wa milele. Kijana tazama shetani ameweka maoteo mbele yako, usiinue macho yako kutazama wanawake waliovaa vibaya maana utawaka tamaa na binti usiwe kichocheo cha tamaa, kinywa chako kisitoe man

VISAKRAMENTI KATIKA KANISA KATOLIKI

Visakramenti ni nini? Ni alama takatifu ambazo kwa sababu zinafanana na Sakramenti, zinaashiria kupatikana kwa matunda ya kiroho kupitia maombi ya kanisa. Visakramenti huwasaidia watu kupokea tunda la msingi la Sakramenti na mazingira mbalimbali ya maisha hutakaswa. Katika maana nyengine: Visakramenti ni shara takatifu zilizoanzishwa na Kanisa ambazo lengo lake ni kuwaandaa watu kupokea tunda la Sakramenti na kutakatifuza mazingira mbalimbali ya maisha. Mfano wa Visakramenti: Misalaba, Medani, Rozari, Skapulari, Maji ya baraka, Matawi yaliyobarikiwa, Majivu yaliyobarikiwa n.k Visakramenti hufanyikaje? Visakramenti hufanyika kwa njia ya Baraka. Ukiwa na Msalaba, Rozari Skapurari etc ambayo haijabarikiwa ni kazi bure haiweizi kufanya kazi yoyote. Ni baada ya kubarikiwa na Padre ndipo Visakramenti hupata pumzi ya uhai ndani yake. Hivyo twasema ni katika kubarikiwa Visakramenti hufanya hai navyo huweza kutubariki. NB: Kila Mkristo mbatiwa naye alibarikiwa hivyo huitwa &quo