Je, ni sahihi kutumia vyombo vya muziki wakati wa Kwaresma?
Utangulizi Msingi wa swali hili ni kwamba, kipindi cha kwaresma ni kipindi cha ukimya, tafakari na majonzi yanayoambatana na kuyawazawaza mateso, kifo na kisha ufufuko wa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristu. Katika wakati kama huu je, ni sahihi kutumia vyombo vya muziki ? Jibu Katika Ibada Katika kujibu swali hili nitatumia "General Instruction of the Roman Missal" ambayo unaweaza kuipata kwa kubonyeza hapa Ukisoma kifungu namba 313 kuhusiana na matumizi ya vyombo vya muziki katika kipindi cha kwaresma inaelezwa kuwa; Vyombo vya muziki vitatumika katika kusaidia uimbaji. Isipokua katika sikukuu na sherehe mfano jumapili ya matawi. Hii ina maana kuwa matumizi ya vifaa vya muziki lazima yawe na lengo moja tu la kusaidia uimbaji. Vifaa kama ngoma, magitaa na vinginevyo vyenye kuonesha hali ya sherehe au tafrija haviruhusiwi katika kipindi hiki, isipokua sikukuu kama ilivyoainishwa. Lakini matumizi ya kinanda (bila ngoma) yanaruhusiwa ili kusaidia uimbaji na tafa...