Je, ni sahihi kutumia vyombo vya muziki wakati wa Kwaresma?

Utangulizi


Msingi wa swali hili ni kwamba, kipindi cha kwaresma ni kipindi cha ukimya, tafakari na majonzi yanayoambatana na kuyawazawaza mateso, kifo na kisha ufufuko wa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristu. Katika wakati kama huu je, ni sahihi kutumia vyombo vya muziki ?

Jibu


  • Katika Ibada


Katika kujibu swali hili nitatumia "General Instruction of the Roman Missal" ambayo unaweaza kuipata kwa kubonyeza hapa

Ukisoma kifungu namba 313 kuhusiana na matumizi ya vyombo vya muziki katika kipindi cha kwaresma inaelezwa kuwa; Vyombo vya muziki vitatumika katika kusaidia uimbaji. Isipokua katika sikukuu na sherehe mfano jumapili ya matawi.

Hii ina maana kuwa matumizi ya vifaa vya muziki lazima yawe na lengo moja tu la kusaidia uimbaji. Vifaa kama ngoma, magitaa na vinginevyo vyenye kuonesha hali ya sherehe au tafrija haviruhusiwi katika kipindi hiki, isipokua sikukuu kama ilivyoainishwa. Lakini matumizi ya kinanda (bila ngoma) yanaruhusiwa ili kusaidia uimbaji na tafakari.

  • Nje ya nyumba ya Ibada
Tunapokua nje ya nyumba za ibada bado tunashauriwa kutumia vyombo vya muziki kwa uangalifu. Ikumbukwe kuwa kipindi hiki kinamuhitaji sana muumini kuweza kupata muda wa tafakari. Ni rahisi sana kutafakari kukiwa na kiwango kidogo cha kelele kuliko kunapokuwapo na kelele nyingi za vyombo vya muziki.

Pamoja na hayo vyombo vya muziki vyaweza kuendelea kutumika (nje ya Ibada) kwa lengo la maandalizi ya kwaya au kujifunza lakini ungalizi wa hali ya juu utumike kuhakikisha haileti usumbufu.



Popular posts from this blog

IFAHAMU SAKRAMENTI YA KITUBIO/UPATANISHO

IFAHAMU SALA YA BWANA (BABA YETU)

NYIMBO ZA BIKIRA MARIA