IFAHAMU SALA YA BWANA (BABA YETU)
Utangulizi Wanafunzi wa Yesu walimuomba awafundishe kusali kama vile ambavyo Yohana aliwafundisha wanafunzi wake kusali. Naye Bwana akawafundisha sala ambaya inatambulika zaidi kama Sala ya Bwana (kwa sababu Bwana mweyewe ndiye aliyeifundisha) aliwaambia msalipo semeni hivi; "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea, usitutie katika vishawishi, Lakini utuopoe na yule muovu" Nyongeza katika sala ya Bwana, Baadaye katika sala ya Bwana maneno yafuatayo yaliongezwa "Kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele Amina." Ukuu wa sala ya Sala ya Bwana Sala hii imepokea heshima na hadhi kubwa kwenye kanisa tangu wakati huo mpaka leo. Mababa wa Kanisa katika mapokeo, mfano Mtakatifu Agoustino anasema; "Zipitieni sala zote zilizo katika maandiko na siamini kama mtakuta humo kitu c...