Posts

Showing posts from 2017

MKRISTO USIOGOPE KIFO JIANDAE KWA KIFO CHEMA

Makala hii ni sehemu ya Kitabu cha Kalamu kwa Vijana ambacho kipo katika hatua za mwisho kuchapishwa.  Haki zote za mwandishi zimehifadhiwa. Utangulizi Kati ya mambo ambayo binadamu tunayaogopa sana mojawapo ni kifo, mwanadamu anaogopa kifo kwa kuwa kwanza kinamtenga na familia yake, ndugu, jamaa marafiki ambao amezoeana nao, pili anaogopa kifo kwa kuwa hafahamu ni wapi anapoelekea, jambo lingine linalowaogopesha watu juu ya kifo ni kuyaacha mambo ya dunia na raha zake ambazo amekua akizihangaikia kwa muda mrefu sana, kifo huogopwa pia kutokana na hukumu kwa wale wanaoamini uwepo wa Mungu na hukumu yake. Mwanadamu anapofariki huku nyuma huacha majonzi na simanzi kubwa haswa kwa wale waliokua wanamtegemea na wote ambao kwa namna moja au nyengine walikua wanafaidika na uwepo wake hapa duniani. Kifo cha kijana mara nyingi huwa ni pigo zaidi, maana ujana ni wakati wa mtu kuchanua na jamii huwa imejiandaa sana kuvuna kutoka kwa vijana, anapofariki kijana jamii huhuzunika zaidi hasw

NYIMBO ZA BIKIRA MARIA

Zifuatazo ni nyimbo mbalimbali za Bikira Maria. Bonyeza nyimbo husika na utaweza kuidownload moja kwa moja AVE MARIA BARAGUMU LA MARIA HERI MARIA HESHIMA TWATOA ISHARA KUBWA JINA LA MARIA LITUKUZWE POTE JINA TUKUFU LA MARIA MAMA WA MWOKOZI TUSIKIE WANAO MARIA MWOMBEZI MIMI NI MTUMISHI WA BWANA MKONO WAKO PAMOJA NA MALAIKA MARIA MSIMAMIZI SALAMU MALKIA WA MBINGU SALAMU MAMA MARIA SALAMU MARIA EE MAMA TUMSIFU MARIA ENYI WANAE ULIZALIWA PASIPOKUA NA DHAMBI UNITETEE KWA MWANAO ZIPENDE NYIMBO ZETU Kwa tatizo lolote wasiliana nasi

Akawanyeshea Mana ili wale

Bonyeza hapa kudownload

Neno kwa Vijana

Vijana tukumbuke mitume na manabii wengi walieneza dini na neno la Mungu angali ni vijana, wakiwa wana nguvu na wenye kustawi, nguvu yao hawakuipeleka katika maasi na machukizo kwa Mungu, bali waliutoa ujana wao machoni pa Mungu wakiitenda kazi yake, na wengine walikufa wakieneza dini tena hawakuona maumivu yoyote kwa sababu walifanya kwa mapenzi ya Muumba wao. Kijana ukiwa bado una nguvu usikubali shetani atumie nguvu yako kumuasi Mungu, Mwili wako usitumike kwa uzinzi wala nguvu yako kwa kuiba kwa kunyang’anya, vipaji vyako visiwe chachu ya maovu kwa kuimba na kucheza isivyompendeza Mungu, kichwa chako na kisitumike kutunga na kuandaa hadithi na michezo yenye uovu. Kumbuka nguvu ya ujana wako yaweza kukupa baraka tele kwa Mungu ukiitumia vizuri bali uitumiapo vibaya itakupeleka katika moto wa milele. Kijana tazama shetani ameweka maoteo mbele yako, usiinue macho yako kutazama wanawake waliovaa vibaya maana utawaka tamaa na binti usiwe kichocheo cha tamaa, kinywa chako kisitoe man

VISAKRAMENTI KATIKA KANISA KATOLIKI

Visakramenti ni nini? Ni alama takatifu ambazo kwa sababu zinafanana na Sakramenti, zinaashiria kupatikana kwa matunda ya kiroho kupitia maombi ya kanisa. Visakramenti huwasaidia watu kupokea tunda la msingi la Sakramenti na mazingira mbalimbali ya maisha hutakaswa. Katika maana nyengine: Visakramenti ni shara takatifu zilizoanzishwa na Kanisa ambazo lengo lake ni kuwaandaa watu kupokea tunda la Sakramenti na kutakatifuza mazingira mbalimbali ya maisha. Mfano wa Visakramenti: Misalaba, Medani, Rozari, Skapulari, Maji ya baraka, Matawi yaliyobarikiwa, Majivu yaliyobarikiwa n.k Visakramenti hufanyikaje? Visakramenti hufanyika kwa njia ya Baraka. Ukiwa na Msalaba, Rozari Skapurari etc ambayo haijabarikiwa ni kazi bure haiweizi kufanya kazi yoyote. Ni baada ya kubarikiwa na Padre ndipo Visakramenti hupata pumzi ya uhai ndani yake. Hivyo twasema ni katika kubarikiwa Visakramenti hufanya hai navyo huweza kutubariki. NB: Kila Mkristo mbatiwa naye alibarikiwa hivyo huitwa &quo

KANISA LINAISHI MAFUNDISHO YAKE – MSAMAHA

Fr. Innocent Bahati Mushi OFMCap Kanisa liko makini juu ya kile ambacho linafundisha. Linajitahidi kadiri iwezekanavyo kutafsiri mafundisho yake kwa matendo. Linafahamu fika kwamba matendo huongea zaidi kuliko maneno matupu. Kanisa kwa lenyewe limekuwa likiomba msamaha kutokana na madhambi na madhaifu ya wanawe. Huu ni utambuzi kwamba Kanisa ni la kimungu lakini pia ni taasisi ya kibinadamu, watu ambao wamejeruhiwa na dhambi ya asili na wana maelekeo ya dhambi. Wakati wa hija, huko nchi takatifu tarehe 23 Marchi, 2000, Papa Yohani Paulo II alienda Yad Vashem, sehemu ya kumbukumbu ya maangamizi ya Waisrael (Holocost). Huko Papa alisema:  “Kama Askofu wa Roma, na Khalifa wa Petro, ninapenda kuwahakikishia Wayahudi wote kwamba Kanisa Katoliki, likisukumwa na nguvu ya ukweli na upendo wa kiinjili, bila kuingiza mambo ya kisiasa ndani yake, linahuzunishwa na kusikitishwa na kitendo cha Wakristo, wa wakati wowote na mahali popote, kuwachukia, kuwatesa na hata kuwaua ndugu Wayahu

AFYA NJEMA – NINI MAANA YAKE? KUELEKEA MSAMAHA

Fr. Innocent Bahati Mushi OFMCap Moja ya jambo ambalo ni kama mwiba katika ngozi ambalo sisi binadamu tunaalikwa kulifanya ni kuwasamehe waovu kwa kuwatendea mema, na kuwasamehe hata yale yanaonekana hayasameheki. Tunapenda kusoma masimulizi ya watu waliofanikiwa kusamehe uovu waliotendewa kwa upendo, lakini hali hiyo inapotusibu sisi wenyewe, kinachoendelea ndani yetu ni hasira, chuki, mfadhaiko, tunaishiwa nguvu kabisa kiasi cha kuchanganyikiwa. Tunatumia nguvu nyingi sana kupambana na uovu ule na kutaka kulipiza kisasi.  AFYA NJEMA – UTAFITI CHUO KIKUU HAVARD Stadi za maisha na tafiti mbalimbali zilizofanywa Havard University  2001 zinaonesha kwamba kama tunataka kuwa na afya njema, kuishi muda mrefu pasipo msongo moyo na mfadhaiko usio na maelezo, ni lazima tujenge utamaduni wa kuachilia maumizo ya zamani na kuwa na mtazamo chanya juu ya wenzetu hata wale wanaoonekana kuwa ni maadui zetu. Katika wema tunashinda mengi, katika ubaya tunaelekea kuzama katika uovu na uadui

IFAHAMU SALA YA BWANA (BABA YETU)

Utangulizi Wanafunzi wa Yesu walimuomba awafundishe kusali kama vile ambavyo Yohana aliwafundisha wanafunzi wake kusali. Naye Bwana akawafundisha sala ambaya inatambulika zaidi kama Sala ya Bwana (kwa sababu Bwana mweyewe ndiye aliyeifundisha) aliwaambia msalipo semeni hivi; "Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea, usitutie katika vishawishi, Lakini utuopoe na yule muovu" Nyongeza katika sala ya Bwana, Baadaye katika sala ya Bwana maneno yafuatayo yaliongezwa "Kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu na utukufu hata milele Amina."  Ukuu wa sala ya Sala ya Bwana Sala hii imepokea heshima na hadhi kubwa kwenye kanisa tangu wakati huo mpaka leo. Mababa wa Kanisa katika mapokeo, mfano Mtakatifu Agoustino anasema; "Zipitieni sala zote zilizo katika maandiko na siamini kama mtakuta humo kitu c

IFAHAMU SAKRAMENTI YA KITUBIO/UPATANISHO

Image
Maana Sakramenti ya kitubio pia huitwa sakramenti ya Upatanisho, ipo katika fungu la sakramenti za uponyaji. Kuna Sakramenti mbili za uponyaji, kitubio na mpako mtakatifu wa wagonjwa. Dhumuni haswa la Sakramenti ya uponyaji ni kuzirejeshea uhai roho zetu pale zinapougua kwa kutenda dhambi. Yesu ndiye tabibu mkuu wa roho zetu naye yu tayari kututibu kila tunapougua. (Katekisimu Katoliki 1420,1421) Sakramenti ya kitubio huhusisha, kutambua makosa, kujuta na kuungama pamoja na kuweka nia ya kutotenda dhambi hiyo tena. Kitubio hutusafisha dhambi tulizozitenda baada ya ubatizo. Tunakumbuka, siku ya ubatizo tulipewa kitambaa cheupe, ikiwa ni ishara ya kuwa sasa tumekuwa wapya. Lakini kadri tunavyosongwa na mambo ya dunia, kitambaa chetu cheupe kinachafuka nacho chahitaji kusafishwa, ndio maana tunapata Sakramenti ya kitubio. Wakati gani unahitaji Sakramenti ya kitubio Kila wakati unapotenda dhambi unahitaji Sakramenti ya kitubio. Usisubiri ukirundika dhambi zako ili

UNGAMA, TUBU KAMA DAUDI (Uchambuzi wa Zaburi ya 51)

Wataalamu wa fasihi wanaeleza kuwa ushairi au utenzi ni namna ambayo binadamu huitumia kueleza hisia zake za ndani kabisa. Ni katika mwangaza huu napenda nikushirikishe utenzi wa Daudi unaopatikana katika Zaburi ya 51. Daudi aliandika utenzi huu baada ya kutenda dhambi kubwa iliyokua chukizo kwa Mungu. Daudi alitumia madaraka yake, kutembea na Bath-sheba mke wa Askari wake (Uria), kisha baada ya hayo Daudi alimuua Uria ili kuificha dhambi yake. Mungu alimtuma Nabii Nathani, aende kwa Daudi kumweleza kuwa amechukizwa na dhambi aliyotenda Daudi. Kwa majuto makuu Daudi alilia mbele ya Bwana Mungu akitubu (2 Saweli 11, 12:1-15) . Zaidi ya hayo aliiandika zaburi hii tuitumiayo sana katika kipindi hiki cha Kwaresima. Uchambuzi wa Zaburi hii ya 51 unalenga kutusaidia kuungama na kutubu katika dhati na unyoofu wa moyo, pia hutupatia mambo ya kuzingatia wakati wa kuungama. Mambo haya nikuelezayo ni muhimu kuyafanya wakati unatafakari, kabla ya kwenda katika kiti

Je wewe ni Simeoni wa Kirene? (Tafakari)

Tunasoma katika Injili ya Mtakatifu Marko 15:21, habari za Simeoni wa Kirene aliyemsaidia Yesu msalaba. Ni mstari mmoja tu, lakini wenye maana kubwa sana katika Imani. Kanisa kwa kutambua mchango wa mstari huu mmoja, umetenga kituo cha tano katika Ibada ya njia ya msalaba, kutafakari fumbo hili kubwa. Nataka nikukaribishe tuutafakari mstari na fumbo hili la Simeoni wa Kirene anayemsaidia Yesu Msalaba. Mazingira ya tukio Simeoni alikua anatoka shambani kuelekea nyumbani kwake. Yamkini hakua anafahamu ni jambo gani linaloendelea wakati ule, au kama alikua anafahamu basi halikua jambo la msingi sana kwake. Maana kama angekua ni mwamini au mwanafunzi wa Yesu Kristo asingekua anatokea shambani wakati ule, lazima angekua katika hali ya huzuni na majonzi. Simeoni yamkini alisogea katika msongamano ule wa safari ya kuelekea Kalivari baada ya kuona mkusanyiko mkubwa wa watu, ni hulka ya binadamu kupenda taarifa. Labda alijongea ili kujua ni nini kinaendelea. Lakini ghafla, anashur

Kwaresima: Jifunze, Tafakari juu ya fumbo la Shamba la Mizabibu (Isaya 5:1-7)

Katika Isaya 5:1-7, Nabii Isaya, anaeleza fumbo fupi kupitia kisa cha shamba la mizabibu. Kisa cha Shamba la Mizabibu? Anaeleza; Mkulima alikua na shamba la mzabibu, mahali pa kilimani penye kuzaa sana, kwa kulijali akalipalilia, akalisafisha, akaweka samadi iliyo nzuri, akalitengenezea na kisima cha maji ndani yake. Akitegemea kuwa litazaa zabibu zilizo njema na safi lakini likazaa zabibu mwitu, zabibu chungu. Kisha anauliza akisema; Je, ni jambo gani nililopaswa kulitenda katika shamba langu la mizabibu na sikulifanya? Mbona nalipotegemea litazaa zabibu safi limezaa zabibu mwitu? Fumbo hili lina maana gani? Mkulima ni Mungu, na shamba la mizabibu ni sisi binadamu kila mmoja kwa nafasi yake. Kazi aliyoifanya mkulima ya kuliandaa shamba la mizabibu ni zawadi, vipawa, na talanta ambazo Mungu ametujalia. Zabibu ni matunda yatokanayo na zawadi, talanta na vipawa ambavyo Mungu ametujalia. Fumbo hili lina uhalisia gani? Katika maisha yetu Mungu ametu

Je, ni sahihi kutumia vyombo vya muziki wakati wa Kwaresma?

Utangulizi Msingi wa swali hili ni kwamba, kipindi cha kwaresma ni kipindi cha ukimya, tafakari na majonzi yanayoambatana na kuyawazawaza mateso, kifo na kisha ufufuko wa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristu. Katika wakati kama huu je, ni sahihi kutumia vyombo vya muziki ? Jibu Katika Ibada Katika kujibu swali hili nitatumia "General Instruction of the Roman Missal" ambayo unaweaza kuipata  kwa kubonyeza hapa Ukisoma kifungu namba 313 kuhusiana na matumizi ya vyombo vya muziki katika kipindi cha kwaresma inaelezwa kuwa; Vyombo vya muziki vitatumika katika kusaidia uimbaji. Isipokua katika sikukuu na sherehe mfano jumapili ya matawi. Hii ina maana kuwa matumizi ya vifaa vya muziki lazima yawe na lengo moja tu la kusaidia uimbaji. Vifaa kama ngoma, magitaa na vinginevyo vyenye kuonesha hali ya sherehe au tafrija haviruhusiwi katika kipindi hiki, isipokua sikukuu kama ilivyoainishwa. Lakini matumizi ya kinanda (bila ngoma) yanaruhusiwa ili kusaidia uimbaji na tafa

ZINGATIA HAYA UNAPOFUNGA KWARESIMA

Utangulizi Moja kati ya mambo yanayoambatana na kipindi cha Kwaresima ni kufunga. Pamoja na hili pia kuna kusali, kutoa sadaka, kufanya toba na kushiriki matendo ya huruma. Katika kipindi hiki waamini tunaalikwa kufunga kama sehemu ya majuto na toba kutokana na dhambi zetu tulizozitenda. Katika  maana pana kufunga ni moja kati ya njia za kutafuta ukaribu zaidi na Mungu. Kufunga ni kujinyima chakula, maji, vitu au mambo ya kidunia kwa utukufu wa Mungu. Sheria juu ya kufunga Ni Amri ya kanisa kufunga siku ya Jumatano ya majivu na kutokula nyama siku ya Ijumaa kuu. Vivyohivyo katika sheria za kanisa, sheria namba 1250 mpaka 1252 zinaeleza kuwa Ijumaa zote pamoja na kipindi cha kwaresima ni siku za toba. Vijana wa kuanzia umri wa miaka kumi na minne mpaka wazee wa umri wa miaka sitini wana wajibu katika kanisa wa kufunga na kujinyima katika siku hizo za toba. Ungalizi wa kanisa na wazazi unahitajika kuwaeleza watoto maana haswa ya kufunga. Hali kadhalika wazee, wajawazito, wa

IFAHAMU JUMATANO YA MAJIVU

Image
“Rarueni mioyo yenu wala si mavazi yenu....” Yoeli 2:13 UTANGULIZI Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa. Ni ishara ya kuanza kwa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu ili kuichukua aibu yetu. Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu. KWA NINI TUNAPAKWA MAJIVU? Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako. Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13 KWA NINI MAJIVU YAPAKWE KATIKA PAJI LA USO NA SI PENGINEPO? Ishara yoyote iwekwayo katika p

Tumekosa Kweli (Kwaresma)

Zaeni Matunda Mema (Tafakari)

Siku ya Ubatizo wangu (Tafakari)

Kiapo Cha Ubatizo (Tafakari)

Jenga Urafiki (Tafakari)

Yesu Wangu Niokoe (Kwaresma)

Yesu Akalia kwa Sauti Kuu (Kwaresma)

Mungu Wangu Mbona Umeniacha (Kwaresma)

Mungu Unihifadhi Mimi (Kwaresma)

Laumu Imeuvunja Moyo wangu (Kwaresma)

Kwa nini Wasimama Mbali (Kwaresma)

Ee Bwana Kumbuka (Kwaresma)

Bwana ni Kinga na Ngome Yangu (Kwaresma)

Bwana Ndiwe Mchungaji Wangu (Kwaresma)

Bwana Kama Wewe (Kwaresma)

Pasipo Makosa (Kwaresma)

Nimekukimbilia (Kwaresma)

Mungu Wangu (Kwaresma)

Mtazame Mwokozi (Kwaresma)

Msalabani (Kwaresma)

Mateso yako (Kwaresma)

Kwa Ishara ya Msalaba (kwaresma)

Kristu amekua mtii (kwaresma)

Kristu Alijinyenyekeza (Kwaresma)

Kabila langu (Kwaresma)

Ee Bwana usikie (Kwaresma)

asiregewe moyowe